Serikali ijayo ya CCM kurasimisha biashara za wafanyabiashara wadogo

GEORGE MARATO TV
0


Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameendelea na mikutano yake kampeni ndani ya jiji la Dar Es Salaam, ambapo akiwa Wilaya ya Ubungo amesema Serikali ijayo ya CCM imedhamiria kwa dhati kurasimisha biashara za Wafanyabiashara wadogo ili wafanye biashara zenye tija




Akiwa katika viunga vya EPZA-Mabibo leo Septemba 29, 2025 wilayani Dkt Nchimbi amewahutubia Wananchi huku akinadi Sera na Ilani ya chama hicho ya 2025-2030 ikilenga kuimarisha sanjari na kupeleka maendeleo kwa Wananchi.





Aidha baada ya kuhutubia Wananchi, Dkt Nchimbi pia alipata nafasi ya kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo pamoja na Madiwani.


 


Dkt.Nchimbi ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 wakipeperusha bendera ya Chama  Cha Mapinduzi (CCM), ambapo mkoa wa Dar es Salaam unakuwa wa 15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za ushindi  wa Kishindo za Mgombea Urais wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan, Wabunge pamoja na Madiwani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top