Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rushwa na Fitina Chanzo cha Kukatwa Wabunge Majimboni


 Hekaheka za mchujo CCM:

Sababu ya wabunge nguli kufyekwa na wajumbe hizi hapa 

*Yadaiwa walikuwa bize na wananchi wakasahau 'kuwaona' wajumbe wa kamati za siasa

*Wajumbe wengine walia kupunjwa mgao


BAADHI ya kamati za siasa za chama cha Mapinduzi CCM za wilaya nchini, zinadaiwa kukiuka taratibu za chama hicho za kuwapata viongozi wa dola kwa madai ya kupokea rushwa, jambo ambalo liliwafanya kuendesha vikao vya mchujo kwa upendeleo mkubwa, chuki na fitna.

Uchunguzi ambao umefanywa katika baadhi ya mikoa nchini, umebaini kuwa baadhi ya viongozi wa kamati hizo hasa wenyeviti na makatibu walinunuliwa kabla ya kuanza kwa vikao hivyo vya mapendekezo kwa wagombea ubunge na udiwani.

Imeelezwa kuwa chanzo cha viongozi hao kununuliwa na baadhi ya wana CCM, waliokuwa tayari wamejipanga kuchukua fomu ni kutokana na baadhi ya wabunge kushindwa kuwajali binafsi badala yake walitumia muda mwingi kwa shughuli za maendeleo pamoja na kuwalinda wajumbe katika maeneo hayo.

Imeelezwa kuwa kutokana na wabunge kushindwa kuwapa 'malezi' iliwalazimu kuingia mikataba na baadhi ya wana CCM walionesha nia ya kugombea ubunge katika maeneo yao hivyo kuwasaliti wabunge walikuwepo madarakani. Hatua ambayo ilizua migogoro kati ya wabunge na viongozi hao.

Mmoja wa wajumbe hao amesema "Kaka sisi ni binadamu, tulienda mkutano mkuu Dodoma Wilaya yetu ina majimbo zaidi ya moja, lakini tumekaa siku zote hatukuona mbunge hata mmoja kutukaribisha chakula na wao walikuwa hapo hapo Dodoma, tulifadhiliwa sana na baadhi ya makada ambao leo wamechukua fomu za ubunge hivyo unatarajia sisi tumpendekeze kwenye kikao chetu?yeye alidhani sisi tunakula madarasa au zahanati zake alizojenga?tumewafyeka ngoja waponee huko vikao vya juu lakini sio kwetu"alisema. mmoja ya kiongozi katika moja ya wilaya mkoani Mara

Aliongeza kuwa "Huwezi kumpendekeza mtu eti kwa vile wananchi wanamhitaji. Je, sisi tufe njaa? Tumesema tupo tayari kwa lolote lakini hatuwezi kuwapendekeza kwa kikao chetu.tunajua 2027 ni vita lakini tumesema tunataka kuonesha mfano"aliongeza

Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo za siasa ngazi ya wilaya ambao pia wamedai kupunjwa mgao wa fedha zilizotolewa na watia nia wamesema pamoja kuwa wameshiriki katika mchezo huo lakini wamejutia kuingizwa katika vita ambayo hawakuitegemea kwa sasa.

"Kweli mimi ni mjumbe tulipewa maelekezo na Mkubwa wetu kuwa kuna fedha tutapata mimi nimeambulia milioni mbali huku viongozi wetu wakigawana milioni 20 kila mmoja,najuta kwa nini nimeshiriki katika kitendo hiki"alisema mjumbe huyo wa kamati ya siasa katika moja ya wilaya mkoa wa Mara.

Kauli za baadhi ya viongozi na wajumbe hao zimeonejana kufanana kwa baadhi ya maeneo nchini jambo ambalo ni hatari na linaweza kusababisha madhara makubwa kwa chama

Mzee Juma Remagwe wa wilaya ya Tarime alisema kuwa vitendo hivyo vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa CCM kwa maslahi binafsi vinaweza kusababisha chuki kwa wananchi kwa kuchaguliwa viongozi wao na kikundi cha watu wachache jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa chama.

"Ndugu mwandishi CCM hii sio ile ya Nyerere kuna viongozi wamepewa nafasi kumbe ni majizi kabisa,unawezaje kuharibu sifa za chama kwa maslahi yako binafsi,hivi kama kingekuwa ndio kikao cha mwisho tungetarajia nini,nadhani ufike wakati mwrmyekiti wa chama awe mkali kwa wahuni kama hawa wanaotumia kofia ya chama kufanya vitendo vichafu kiasi hiki,mwenyekiti mzima unatembea na mtia nia mwaka mzima,unagawa rushwa za mtia nia huku mbunge yupo madarakani,lakini hatukuona hatua zimechukuliwa,sijui vyombo vyetu vya usalama havioni hili ni hatari kwa maisha ya chama tawala'alisema

Taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa baadhi ya wabunge wengi wanamaliza muda wao wameshindwa kupendekezwa na vikao vya kamati za siasa za wilaya na zile za mkoa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo hizo zilizoelezwa hapo juu.

BAADHI ya kamati za siasa za chama cha mapinduzi CCM za wilaya nchini zinadaiwa kukiuka taratibu za chama hicho za kuwapata viongozi wa dola kwa madai ya kupokea rushwa jambo ambalo liliwafanya kuendesha vikao vyao kwa upendeleo mkubwa,chuki na fitna.

Uchunguzi ambao umefanywa katika baadhi ya mikoa nchini umebaini kuwa baadhi ya viongozi wa kamati hizo hasa wenyeviti na makatibu walinunuliwa kabla ya kuanza kwa vikao hivyo vya mapendekezo kwa wagombea ubunge na udiwani.

Imeelezwa kuwa chanzo cha viongozi hao kununuliwa na baadhi ya wana ccm walikuwa tayari wamejipanga kuchukua fomu ni kutokana na baadhi ya wabunge kushindwa kuwajali binafsi badala yake walitumia muda mwingi kwa shughuli za maendeleo pamoja ma kuwalinda wajumbe katika maeneo hayo.

Imeelezwa kuwa kutokana na wabunge kushindwa kuwapa maelezi iliwalazimu kuingia mikataba na baadhi ya wana ccm walionesha nia ya kugombea ubunge katika maeneo yao hivyo kuwasaliti wabunge walikuwepo madarakani hatua ambayo ilizua migogoro kati ya wabunge na viongozi hao.

"Kaka si ni binadam,tulienda mkutano mkuu Dodoma wilaya yetu inajimbo zaidi ya moja,lakini tumekaa siku zote hatukuona mbunge hata mmoja kutukaribisha chakula na wao walikuwa hapo hapo Dodoma,tulifadhiliwa sana na baadhi ya makada ambao leo wamechukua fomu za ubunge hivyo unatarajia sisi tumpendekeze kwenye kikao chetu?yeye alidhani sisi tunakula madarasa au zahanati zake?tumewafyeka ngoja waponee huko sio kwetu"alisema mmoja ya kiongozi katika moja ya wilaya mkoani Mara

Aliongeza kuwa"Huwezi kumpendekeza mtu eti kwa vile wananchi wanamhitaji, je sisi tufe njaa? Tumesema tupo tayari kwa lolote lakini hatuwezi kuwapendekeza kwenye kikao chetu.

Mjumbe huyo alisema wanafahamu fika kwamba huenda uamuzi wao ukawasababishia machungu katika uchaguzi ujao wa viongozi wa Chama mwaka 2027.

"Tutunajua 2027 ni vita lakini tumesema potelea mbali, tunataka kuonesha mfano"aliongeza.

Hata hivyo katika sakata hilo imebainika kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hizo za siasa ngazi ya wilaya kupunjwa mgao wa fedha zilizotolewa na watia nia.

 Wamesema pamoja kuwa wameshiriki katika mchezo huo lakini wamejutia kuingizwa katika vita ambayo hawakuitegemea kwa sasa.

"Kweli mimi ni mjumbe tulipewa maelekezo na mkubwa wetu kuwa kuna fedha tutapata mimi nimeambulia milioni mbili huku viongozi wetu wakigawana milioni 20 kila mmoja, najuta kwa nini nimeshiriki katika kitendo hiki"alisema mjumbe huyo wa kamati ya siasa katika moja ya wilaya mkoa wa Mara.

Kauli za baadhi ya viongozi na wajumbe hao zimeonekana kufanana kwa baadhi ya maeneo nchini, jambo ambalo ni hatari na linaweza kusababisha madhara makubwa kwa chama hicho kinachotawala 

Mzee Juma Remagwe wa wilaya ya Tarime alisema kuwa vitendo hivyo vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa CCM kwa maslahi binafsi vinaweza kusababisha chuki kwa wananchi kwa kuchaguliwa viongozi wao na kikundi cha watu wachache. Alisema hatua hiyo inaweza kuleta madhara makubwa kwa chama siku za usoni.

"Ndugu Mwandishi CCM hii sio ile ya Nyerere kuna viongozi wamepewa nafasi kumbe ni majizi kabisa, unawezaje kuharibu sifa za chama kwa maslahi yako binafsi,hivi kama kingekuwa ndio kikao cha mwisho tungetarajia nini? Nadhani ufike wakati Mwenyekiti wa chama awe mkali kwa wahuni kama hawa wanaotumia kofia ya chama kufanya vitendo vichafu kiasi hiki. Mwenyekiti mzima unatembea na mtia nia mwaka mzima,unagawa rushwa za mtia nia huku mbunge yupo madarakani, lakini hatukuona hatua zimechukuliwa, sijui vyombo vyetu vya usalama havioni? Hii ni hatari kwa maisha ya chama."'alisema.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa baadhi ya wabunge wengi wanaomaliza muda wao wameshindwa kupendekezwa na vikao vya kamati za siasa za wilaya na zile za mkoa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo hizo za rushwa.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM siasa, Uenezi na Mafunzo Amos Makala alipotafutwa na Mwandishi wa habari hii ili aweze kuzunguzia tuhuma hizi na hatua zinazoweza kuchukuliwa endapo ikithibitika viongozi hao kukiuka taratibu na miongozo ya chama, hakuweza kupatikana baada ya simu yake kuita bila majibu. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi haukuweza kujibiwa. Juhudi za kumtafuta bado zinaendelea.

Tayari CCM kupitia kwa viongozi wake wakuu, wamesikika mara kadhaa wakionya vikao vya maamuzi kutenda haki na wajumbe wake kujiepusha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili, upendeleo na rushwa wakati wote wa kujadili wana CCM waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za dola.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...