Warundi 467 waliokuwa uhamishoni katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma magharibi mwa Tanzania ndio ambao wameripotiwa kurejea nchini mwao kwa hiari ndani ya miezi sita iliyopita.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkoani Makamba mratibu mipango wa kuwarejesha Warundi kanda ya mashariki mwa Burundi,Antoine Ntirandekura amebainisha kuwa idadi hiyo ni ndogo zaidi ikilinganishwa na ambao walikuwa wanatarajia kuwapokea.
Amesema kuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiwapokea wanawake na watoto wanaorejea kutoka katika kambi za Nyarugusu na Nduta,akitoa kwa Warundi waliopo uhamishoni kurejea nchini mwao kutokana na usalama kuimarika.
Warundi walikimbia machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Burundi, mwezi Aprili mwaka 2015 baada ya aliyekuwa Rais wa Burundi kwa wakati huo, Pierre Nkurunziza kutaka kuwania kwa mara ya tatu uongozi wa nchi hiyo kinyume cha katiba ya Burundi.




Comments
Post a Comment