Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Bara Mhe. Joshua Mirumbe leo tarehe 18/06/2025 ametembelea Mradi wa Tangi na Mtandao wa Usambazaji Maji Kata ya Wariku na kuipongeza sana Mamlaka ya Maji (BUWSSA) chini ya Usimamizi wa Mkurugenzi Bi. Esther Gilyoma kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Mamlaka, vifaa vilivyobaki kwenye miradi mingine na kuanzisha mradi huo ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama.
Sambamba na hilo Mhe. Joshua Mirumbe amewashukuru Wakandarasi kwa kuanza kazi na kufikia asilimia 37 ya utekelezaji wa mradi.
Mwisho, Mheshimiwa Mirumbe amewashukuru wakazi wa Kata ya Wariku kwa kutoa eneo la ujenzi wa Tangi hii inaonyesha uzalendo kwa taifa letu.






Comments
Post a Comment