Tanzania na Finland zinasherehekea miaka 60 ya ushirikiano uliojengwa katika misingi ya urafiki, maelewano na kuheshimiana. Ziara hii ni hatua ya nchi zetu kuendelea kuimarisha ushirikiano huo ambao matunda yake tumeendelea kuyaona katika sekta za utawala bora, elimu na utunzaji mazingira.
Tumejadili na kukubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta zinazogusa maisha ya watu wetu kama vile uchumi wa buluu, nishati, elimu na teknolojia. Aidha, nimetumia nafasi hii kuwakaribisha wafanyabiashara alioambatana nao kuangalia fursa za biashara na uwekezaji nchini.








Comments
Post a Comment