Mbunge Mathayo Aendelea na Ziara Kata Kwa Kata Akitoa Taarifa ya Utekeleza wa Ilani ya Ccm na Mafanikio Yake
Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameendelea na ziara yake ya kufika Kata kwa Kata kuelezeautekelezaji wa ilani katika kipindi cha 2020 hadi 2025
Katika ziara hiyo mbunge huyo anakutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) na viongozi mbalimbali.
Hadi sasa ameshazifikia Kata 10 kati ya Kata 16 zilizopo jimbo la Musoma mjini zikiwa ni Nyakato,Kitaji,Mukendo,Bweri,Nyamatare,Buhare,Iringo,Kwangwa,Nyasho na Mwigobero.
Katika mikutano hiyo,Mbunge huyo amewataka wajumbe hao na wanachama wa CCM kutembea kifua mbele kutokana ilani kutekelezwa kwa asilimia kubwa hata kabla ya kumalizika kwa mwaka 2025
Akiwa Kata za Kwangwa,Nyasho na Mwigobero leo machi 2 amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amegusa kila sekta kwa kutoa fedha nyingi za miradi iliyotekelezwa ambayo ipo iliyokamilika,inayoendelea na mingine ya kimkakati itaanza hivi karibuni.
Katika sekta ya afya amesema kwa zile huduma za kibingwa zinapatikana hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lakini zipo zahanati,vituo vya afya na hospitali ya Wilaya ambako kote huduma za afya zinatolewa kwa ufanisi.
Akipokelewa kwa shangwe Kata ya Nyasho Mathayo amesema licha ya kufikiwa na huduma mbalimbali za kijamii lakini ujio wa mradi mkubwa wa ujenzi wa soko la Ä·isasa la kimkakati linakwenda kuinua uchumi wa wananchi wa Kata hiyo na jimbo zima la Musoma mjini.
Amesema tayari taratibu za ujenzi wa soko hilo umeanza na kuomba wakandarasi kupewa ushirikiano na wana CCM kufatilia utekelezani wa ilani.
Akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Mwigobero na viongozi waliohudhuria amezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo miundombinu iliyotekelezwa kwenye Kata hiyo zikiwemo barabara za kiwango cha lami.
Amesema anachokipigania kwa sasa ni kuona wananchi wanakuwa na uchumi na kumiliki fedha mfukoni kwa kufatilia ufunguaji wa viwanda na shughuli nyingine za kujipatia kipato.
" Niwashukuru sana wana CCM kwa maeneo yote ambayo nimeshayafikia kwa kujitokeza kwa wingi kusikiliza utekelezaji wa ilani.
" Naomba tutembee kifua mbele na kumsemea Rais Dkt.Samia namna utekelezaji uliofanyika kwenye miradi ambayo inaonekana kwa macho",amesema.
Diwani wa Kata ya Mwigobero Mariam Sospeter amemshukuru mbunge huyo kwa ufatiliaji wake na kupelekea kufikiwa na miradi mingi ndani ya jimbo.
Naibu Meya wa manispaa ya Musoma na diwani wa viti maalum Naima Minga amesema yale aliyoyafanya mbunge Mathayo anapaswa kuungwa mkono na wale wanaombeza waendelee kupuuzwa.





Comments
Post a Comment