Picha mbalimbali zikimuonesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akishiriki shughuli ya mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Namibia, Baba wa Taifa hilo na kiongozi wa mapambano ya kupata uhuru wa nchi hiyo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, yaliyofanyika katika eneo la makaburi ya mashujaa, jijini Windhoek, na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji, kutoka ndani na nje ya Namibia, wakiongozwa na Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba, pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa Namibia, tarehe 1 Machi 2025.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.







.jpg)



Comments
Post a Comment