Waziri wan Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu na Mbunge wa Chalinze Mhe, Ridhiwani Jakaya Kikwete leo Februari 9 2025 ametolea ufafanuzi Miradi miwili ya ujenzi wa Barabara ambazo zipo chini ya TANROADS ikiwa ni pamoja na Barabara inayoanzia Mandera hadi Saadani pamoja na Barabara ya Afrika Mashariki ambayo inatokea masuguru hadi pangani.
Ameyasema hayo alipofanya ziara katika Kata ya Mkange na kuzungumza na Wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani. Pia amewahakikishia kuwa wale wote ambao maeneo yao yamepitiwa na Barabara hiyo watalipwa stahiki zao kwa kukamilisha nyaraka muhimu.
Aidha Mhe Ridhiwani amewaasa wananchi kuacha kuzungumza kwa kukisia kwani serikali inatambua zoezi la ulipaji wa fidia kwenye maeneo yanayomilikiwa na wananchi pia amewakabidhi rasmi wataalamu kutoka Tanrods ambao watasimamia zoezi la kulipa fidia wananchi hao .
Kwaupande wake Mthamini wa Mkoa wa Pwani Tanrods Bi Maria Iranda ametaja baadhi ya vigezo vya kupata fidia huku akiwakumbusha wananchi kuwa wapo baadhi yao wamepata fedha kama fidia na kusema kuwa itarahisisha zoezi hilo.pia ametaja vitu vinavyotakiwa kuambatanishwa ambavyo utaratibu wake utabandikwa kwenye ofisi za vijiji ili wavitambue vigezo hivyo.
Nae Diwani wa kata Mkange Mhe, Mohamed Geregeza amempongeza Mhe Mbunge Ridhiwani kwa uwepo wake kwani amefanikisha ujenzi wa shule ya sekondari mkange ambapo imepatiwa hekari 100 ambazo ni fedha za mfuko wa jimbo .
Pia Mhe Mbunge amegawa Shilingi Milioni moja kwa kikundi cha uchimbaji wa Kokoto ambazo aliahidi kukipatia Fedha kikundi hicho alipotembelea katika kijiji cha kwamakulu kilichopo kata ya mkange na kuwaona wananchi wakijipatia kipato kwa kuchimba kokoto wakiwa na vifaa vichache.
Katika ziara hiyo Mhe Ridhiwani amewakumbusha wananchi kujitokeza kushiriki katika kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura

.jpg)
Comments
Post a Comment