Utendaji kazi na bidii vyampandisha cheo askari mmoja wa Jeshi la Polisi Mara

GEORGE MARATO TV
0

 

Na Ada Ouko,

Mara.


KAMANDA wa jeshi la polisi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) Pius Lutumo amemvisha cheo cha sajenti polisi kata wa kata ya Ikoma wilayani Serengeti Koplo Emmanuel Kisiri.

Wadhifa huo umetolewa baada ya kuonyesha bidii na jitihada kubwa katika utendaji wake wa kazi Koplo Kisiri ambaye ni polisi wa kata hiyo amepewa wadhfa huo leo february 4 mwaka huu 2025 katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia Kamnyonge Manispaa ya Musoma mkoani hapa.

Aidha baada ya kumvisha cheo hicho kamanda Lutumo amesema kuwa askari huyo anapaswa kuwa mfano wa kuigwa, na kwamba ushirikiano wake na kujiweka karibu zaidi na jamii anayoihudumia sanjari na wadau mbalimbali ndio umempelekea kupata cheo hicho.


"Kutokana na jitihada alizozionyesha Koplo Emmanuel Kisiri ni dhahiri kuwa ana uwezo wa kuongoza hivyo anastahili kutunukiwa cheo cha sajenti" amesema Kamanda Lutumo.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top