Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Kutunga Sera Na Sheria Ili Kuharakisha Matumizi Ya Nishani Safi Nchini-Rais Samia


 Na MASHAKA MHANDO, Mkinga 

Na Hadija Bagasha Tanga, 

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakwenda kutunga sera na sheria ili kuharakisha mkakati wa matumizi ya nishati safi na kuweza kufikia lengo la watumiaji asilimia 80 ifikapo 2030.

Rais Dkt Samia ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa nishati safi ya kupikia na ugawaji wa mitungi ya gesi kwa wananchi Wilayani Muheza Mkoani Tanga.

Rais alisema kuwa sera hizo rafiki ambazo wanakwenda kuzitunza zitawezesha ushiriki wa sekta binfsi na makampuni yanayojihusisha na uzalishaji wa nishati safi ya kupikia kwa bei nafuu. 

Alisema dhamira ya sasa kama tukiendelea kutumia kuni na mkaa kama nishati kuu ya kupikia tunakwenda kuwa na majanga ambayo yatasababisha kukauka kwa vyanzo vya maji kutokana na ukataji wa miti lakini pia upo uwezekano mkubwa wa kupata maradhi ya kifua kutokana na matumizi ya kuni. 

"Kwasasa tulisema asilimia 80 ya watu wetu ikifika 2030 wawe na nishati safi ya kupikia na kwasasa tuko chini ya asilimia hiyo lakini kwa kasi tunayoendelea nayo nina hakika kabla ya kufikia 2030 tutakuwa tumefikia lengo tulilojiwekea kwenye mkakati wetu, "alisisitiza Rais Dkt Samia. 

"Kukiwa na majanga kama vile ukame upatikanaji wa vyakula unakuwa shida na kusababisha ukosefu wa chakula pamoja na ukosefu wa maji kutokana na kuharibu miti iliyopo karibu na vyanzo vya maji hivyo lengo la kampeni hii ni kuhifadhi misitu ili kuweza kupata maji na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia Nchi, "alisema Rais Dkt Samia. 

Aidha Rais Dkt Samia aliiagiza Wizara hiyo kuendelea kusimamia vizuri huku akiwataka REA kuendelea na mkakati huo ambapo amesema Serikali itaendelea kutunga sera na sheria zitakazowafanya waendelee haraka na mkakati huo. 

Katika hatua nyingine Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alisema awali wakati akimteua mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA kuwa Naibu Waziri pamoja na Nikki wa pili kuwa Mkuu wa wilaya, watu hawakumwelewa lakini vijana hao wanafanya vizuri katika nafasi.

MwanaFA ni Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo ambaye Rais amemwelezea kuwa amekuwa akifanya vizuri kuongea na vijana wenzie wasanii.

Akitoa taarifa fupi mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema kuwa serikali imetoa mitungi ya gesi (LPG) 400,445 kwa ajili ya kusambazwa katika wilaya zote nchini, ambapo kila wilaya inapokea wastani wa mitungi 3,255.

Kwa wilaya ya Muheza, Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa, mitungi hiyo imesambazwa na wananchi wameinunua kwa wingi kutokana na bei yake nafuu ya Shilingi 16,000 kwa mtungi mmoja, ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kupunguza gharama za matumizi ya mwanzo kwa wananchi.

Katika awamu ya kwanza ya mpango huo, jumla ya mitungi 99,000 inasambazwa kote Tanzania Bara na Zanzibar. 

Naibu Waziri huyo wa Nishati ameongeza kwa kusema kuwa, serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inahakikisha upatikanaji wa majiko kwa bei ya ruzuku ili kuwawezesha wananchi kutumia nishati mbadala kwa gharama nafuu.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, kwa lengo la kulinda mazingira na kuboresha maisha ya wananchi.

Naibu Waziri wa Habari, utamaduni sanaa na michezo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma (MwanaFA) amepongeza juhudi za Rais Samia katika kuleta maendeleo Wilayani Muheza akisisitiza kuwa miaka minne ya uongozi wake imeleta mafanikio makubwa zaidi ya kipindi cha miaka 46 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Wilaya hiyo mwaka 1974.

Aidha MwanaFA amemuomba Rais Dkt Samia kujenga soko la kitaifa la machungwa wilayani humo akitoa sababu kuwa wilaya hiyo ndio mzalishaji mkubwa wa machungwa Nchini. 

Naibu Waziri Mwinjuma ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto kubwa katika ununuzi wa machungwa wikayani Muheza kwani madalali wengi wamekuwa wakinunua pasipo utaratibu mzuri. 

"Mheshimiwa Rais sisi ndio wazalishaji wakubwa wa machungwa kwa miaka yote na wazalishaji wakubwa wa viungo lakini tuna matatizo ya kutokuwa na soko linalofahamika ningeomba kwako mheshimiwa Rais tujengewe soko kubwa la kitaifa la machungwa hapa Muheza kwakuwa sisi ndio wazalishaji wakuu lakini hali kadhalika na soko la kitaifa la mazao ya viungo kwa vile sisi ni wazalishaji wakuu, "alisema MwanaFA. 

"Changamoto hii kwenye upande wa machungwa sababu wakulima wanawekeza madalali wanakuja na kununua machungwa yaliyopo mtini kipindi hiki na kununua machungwa yaliyopo mtini kwenye misimu mitatu ijayo ambayo inawasababishia wakulima wetu umasikini mkubwa, "alisisitiza na kuongeza kuwa

"Nina hakika tukipata soko la kitaifa la machungwa hapa kwanza litadhibiti uporomokaji wa bei na kuhakikisha wakulima wetu mazao yao hayaharibiki baada ya kuvuna na kuyatoa kwa bei ya kutupa, "alisisitiza MwanaFA. 

Mchana Rais akiweka jiwe la msingi la kiwanda cha saruji 

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Stanslaus Nyongo amesema kufuatia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali imefuta tozo 374 ili kuondoa kero kwa wawekezaji.

Mbali na tozo, amesema baadhi ya sheria pia zimefutwa na nyingine kurekebishwa zikiwemo sheria 62, na hivyo kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Nyongo ameyasema hayo leo Februari 27, 2025 wakati wa mwendelezo wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga, ambapo Rais amefanya ufunguzi rasmi wa mradi wa awamu ya pili ya Kiwanda cha Chokaa na Saruji (Maweni Limestone) kilichopo Jijini Tanga.

Ameongeza kuwa katika mkutano wa Bunge uliopita, imepitishwa sheria ya kuunganisha taasisi mbili za TIC na EPZA zinazowahudumia wawekezaji wa nje na ndani ili kuanzisha mamlaka ya kushughulikia wawekezaji.

Sheria hiyo pia itaruhusu kuanzisha kituo maalumu cha kukaribisha wawekezaji kwa maana ya usajili na kuwatambua kama wawekezaji wa kimkakati.

Vile vile sheria hiyo imelenga kuanzisha Benki ya Ardhi ili wawekezaji wanapokuja Tanzania wakute sehemu ambazo zipo tayari kwa ajili ya uwekezaji.

Akiweka jiwe la msingi wa mradi wa Maji wa Rais ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushiriki na taasisi nyingine kulinda na kutunza vyanzo vya maji Ili miradi ya maji inayotekelezwa iweze kuwa endelevu

Maelekezo hayo ameyatoa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika stend ya wilaya ya Mkinga mara baada ya kumaliza uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Maji Mkinga - Horohoro ambao unatumia chanzo cha Bwawa la Mabayani.

Amesema kuwa Ili mradi huo uweze kuwa endelevu ni muhimu kudhibiti shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji vilivyopo kwenye mkoa huo 

"Ujenzi wa Mradi huu unatokana na changamoto kubwa ya maji kuwa na chumvi katika ukanda wa vijiji vya mwambao wa bahari. Hivyo, Mradi huu una lengo la kuboresha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi zaidi ya 57,334 wa kata 10 katika vijiji 37 vilivyopo pembezoni mwa barabara ya Tanga -Horohoro pamoja na wananchi wa eneo la Horohoro Mpakani"amesema Rais Samia 

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya maji Mwajuma Waziri amesema kuwa Utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia 45 ambapo usanifu wa mradi mzima umekamilika na kazi zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

"Tayari Bomba kubwa za umbali wa km 37 zimeletwa eneo la Mradi, na bomba zenye urefu wa km 25.5 zimelazwa sambamba na Ujenzi wa matanki mawili ya maji yenye mita za ujazo 200 na 250 umekamilika

Pia amesema kuwa Ujenzi wa matanki matatu ya maji yenye mita za ujazo 500 umefikia asilimia 95, naUjenzi wa matanki matano ya maji yenye mita za ujazo 100 umefikia asilimia 90.

Gharama ya mradi wa maji Mkinga-Horohoro unatekelezwa kwa kutumia fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) na utagharimu jumla ya shilingi 35,472,451,838.59 ambapo mpaka sasa fedha zilizolipwa kwa Mkandarasi ni shilingi 11,320,867,775.79.

Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama wananchi zaidi ya 57,334 waishio katika vijiji 37 vya Wilaya ya Mkinga ambao kwa sasa wanapata huduma ya maji kutoka mbali na maeneo yao na ambayo si salama.

Rais aliwataka wananchi wa Mkinga kumuunga mkono mbunge Dastan Kitandula ambaye ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kutokana na kazi kubwa anayofanya ya kusaidia serikali katika sekta ya utalii.

"Mbunge wenu msipomuona mjue ananisaodia kazi katika sekta ya utalii mnajua nilikuwa na filamu Ile ya Royal Tour Sasa viongozi wa Wizara akiwemo mbunge wenu wanahangaika kuhakikisha watalii wanakuja nchini kwetu,"alisema Rais.

Rais Leo atakuwa na mkutano mkubwa wa majumuisho katika uwanja wa mkutano ambako atahutumia mamia ya watu wa Tanga akiwa anahitimisha ziara yake.














Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...