Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mzee Stephen Masato Wasira amefika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo tarehe 10 Februari 2025 kwa ajili ya kumjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Mara Mzee Christopher Mwita Gachuma (MNEC).
Mzee Wasira amefika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kumjulia hali MNEC Gachuma aliyepata ajali jana tarehe 09 Februari 2025 baada ya gari yake kupinduka na kuacha njia jana katika Eneo la Rung'abure Wilayani Serengeti akiwa njiani kuelekea kwenye mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Stephen Wasira akitokea Wilayani Tarime kuelekea Serengeti.
Mzee Wasira amemuombea afya njema na uponyaji wa haraka MNEC GAachuma ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kila siku ya ujenzi wa Taifa.


Comments
Post a Comment