Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(TANAPA)imetangaza kufungwa kwa muda kwa Kiwanja cha ndege cha Seronera Kilichopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Afisa uhifadhi mkuu,Kitengo cha Mawasiliano (TANAPA) Catherine Mbena imeeleza kuwa Kiwanja cha ndege Seronera kitafungwa kwa muda wa siku tano kuanzia Februari nane hadi 12 mwaka huu kwa ajili ya kupisha ukarabati unaoendelea kwenye Kiwanja hicho.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo,katika kipindi hicho ndege hazitaruhusiwa kutua au kuruka kwenye kiwanja cha ndege cha Seronera.
Hata hivyo,TANAPA imeuhakikishia Umma hususani Wadau wa utalii kuwa Viwanja vingine sita vya ndege vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti vitaendelea kufanya kazi kama kawaida katika kipindi hicho.