Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jk:Bukombe Yatekeleza Ilani Ya Ccm Kwa Kishindo



📌 Rais Samia aleta mapinduzi ya maendeleo Geita

📌 Rais Mstaafu Kikwete asema Watanzania wana deni kwa Rais Samia mwezi Oktoba 

📌 Wanachama wa CCM waaswa kuzingatia maslahi ya Chama

📌 Dkt. Biteko apongezwa usimamizi wa miradi ya maendeleo


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameupongeza uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bukombe kwa Mkutano Mkuu Maalum wa kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Bukombe kwa mwaka 2020-2025.

Rais Mstaafu Kikwete ametoa pongezi hizo leo Februari 8, 2025 wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika Kata ya Igulwa, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.

“ Nawapongeza kwa kuandaa Mkutano huo kwa kuwa unakidhi takwa la katiba ya CCM kwa kuwa inawezesha kupima mlipotoka, mlipo na mnapokwenda. Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la 2022 katika Ibara ya 72 (1) inatambua kuwa Mkutano Mkuu ni kikao kikubwa cha Chama katika ngazi ya wilaya, aidha Ibara ya 74 imetamka kazi za msingi za Mkutano huu kuwa ni kuzungumza mambo yote yanayohusu ulinzi na usalama na maendeleo kwa ujumla katika wilaya.”Amesema Rais Kikwete.

Ameendelea kwa kuwasihi wanachama wa CCM kudumisha umoja na mshikamano “ Wekeni mbele maslahi ya Chama chetu, watajitokeza watu mbalimbali kuja kugombea nafasi mbalimbali wapokeeni lakini wakitokea wenye maneno tu waambieni sie tunataka maendeleo sio maneno"

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM Bukombe amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizosaidia utekelezaji wa idadi kubwa ya miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo.

“Nyie wenyewe mmeona yaliyofanyika Bukombe ni mengi sana na hakuna mkoa wilaya au jimbo ambalo halikuguswa na Rais Samia. Hii ndio sababu ya msingi  iliyofanya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika Dodoma Januari mwaka huu  kumchagua kuwa mgombea wa chama chetu kwa nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,” amesema Rais Kikwete.

Amebainisha kuwa miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa inaonekana na ina faida kwa wananchi huku akieleza jitihada za Dkt. Biteko za kuleta maendeleo katika Jimbo hilo. “ Naomba kuwahakikishia kuwa hamkufanya makosa kumpa kura zenu Dkt. Biteko, naomba  niwaambie kuwa  mambo haya mazuri ya Bukombe yasingetokea kama msingemchagua Dkt. Biteko.”

Aidha, Rais Kikwete amewaasa wananchi wa Bukombe kuwachagua wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ili kuendeleza miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo.

Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu Kikwete amemshukuru na kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mzuri wa nchi na kuwa nchi imetulia na ina amani na maendeleo yanaonekana katika kila eneo.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Bukombe kwa mwaka 2020 - 2025 amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo. 

“ Nianze kwa kusema kwa yote yaliyotekelezwa katika Jimbo hili yametokea  kwa sababu ya matashi mema ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatupenda  sana wananchi wa Bukombe, kwa kipindi ambacho nimekuwa mbunge nimeona  ametoa fedha nyingi  sana kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Jimbo leo,” amesema Dkt. Biteko. 

Vilevile, amesema kuwa Rais Samia ameridhia ujenzi wa barabara ya kutoka Ushirombo hadi Katoro kwa kiwango cha lami na kuwa mkandarasi anatafutwa kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Bukombe inatarajia kutekeleza mradi mkubwa wa nishati ya umeme katika Kata ya Busonzo ambao utazalisha megawati 5 zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa.

Awali akiwasilisha taarifa ya miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM  kwa njia ya makala ya picha jongefu, Dkt. Biteko ametaja miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, huduma za afya, maji, usambazaji wa nishati, ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara na matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari.

Katika sekta ya nishati, makala hiyo inaeleza kuwa huduma ya usambazaji umeme imefika katika vijiji vyote 64 vya Jimbo hilo ili kuendelea kukuza fursa za uwekezaji na kukuza uchumi kwa wananchi. 

Katika sekta ya elimu, sehemu ya makala hiyo inataja miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Bulumbaga wenye gharama ya Sh. 40,000,000.00; ujenzi wa vyumba nane vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Msonga- Ikuzi (Mpya) wenye gharama ya Sh. 160,000,000.00 na ujenzi wa matundu ya vyoo ishirini na nane katika shule ya msingi Msonga wenye gharama ya shilingi milioni 47,439,000,00.

Aidha, katika sekta ya afya, ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na uboreshaji wa hospitali ya wilaya umesaidia kuboresha huduma za afya katika hospitali  na kuboresha hali za afya za wananchi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ukamilishaji wa Zahanati ya Kagwe kwa gharama ya Sh. 50,000,000.00., ukamilishaji wa Zahanati ya Lyambomgongo kwa gharama ya Sh. 50,000,000.00 na ujenzi wa Zahanati ya Ishololo kwa gharama ya Sh. 101,223,889.86.

Aidha, miradi mingine iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao ya kilimo Msangila kwa gharama  ya Sh. 993,314,906.24, uchimbaji wa kisima kirefu katika kijiji cha Namonge Sh.16, 348,900.00 na matengenezo ya sehemu korofi katika barabara ya Uyovu - Namonge – Namarandula (1.50Km) kwa gharama ya Sh. 90,161,000.00.

Sambamba na hayo, Dkt. Biteko amewashukuru madiwani wote wa Jimbo lake kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo katika maeneo yao huku akiwahakikishia kuendelea kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi wao.


Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigella amempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa  jitihada alizofanya wakati wa uongozi wake kwa kujenga msingi mzuri wa kuhakikisha watoto wanapata elimu nchini.

“ Katika uongozi wa Rais Samia tumejenga shule mpya 150 na wakati  ule unatengeneza Ilani Mhe. Rais Kikwete  uliona mzigo kwa wazazi kusomesha watoto na sasa katika uongozi wa Rais Samia kila mwezi tutapokea shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kusomesha  watoto,” amesema Mkuu wa Mkoa Shigella.

Ameongeza  “ Rais Samia ametuleta magari  15 ya kubeba wagonjwa mahututi ambayo tumeyagawa katika hospitali zetu na vituo vya afya. Mkoa wetu pia umepata zaidi ya dola milioni 165 zitakazosaidia kupeleka maji  Chato, Wilaya ya Geita na vijijini, hivyo kufikia malengo ya Serikali ya kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa jamii.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe, Matondo Luhonja amesema kuwa Mbunge wa Bukombe, Dkt. Biteko amekuwa kiongozi msikivu, makini na mwenye ushirikiano na wananchi wake na hivyo mafanikio hayo ya utekelezaji yamechangiwa pia  na uongozi wake mzuri.

Mkutano huo Mkuu wa CCM Bukombe umehudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Bukombe uliambatana na burudani kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmonize.









Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...