Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Mkutano wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika Kuhusu Kilimo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2025 ameshiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika ambapo alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda.
Awali Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia Tamasha la Kahawa Afrika (Africa Coffee Festival) lililolenga kuhamasisha uongezaji thamani katika mazao yanayolimwa Afrika likiwemo zao la kahawa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini mbele ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kushoto) na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya kushuhudia Tamasha la Kahawa Afrika (Africa Coffee Festival) lililolenga kuhamasisha uongezaji thamani katika mazao yanayolimwa Afrika likiwemo zao la kahawa.
Tukio hilo lilifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda ambako alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika, Januari 11, 2025.





Comments
Post a Comment