Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mhe Vedastus Mathayo Leo 14/01/2025 amekabidhi madawati 50 na meza 50, Shule ya Sekondari Mwiyale iliyopo kata ya Kigeara katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.
Dawati na meza hizo vimekabidhiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma, Mhe Williamu Patrick Gumbo kwa niaba ya mbunge Mathayo ambaye kwa sasa yupo mjini Bungeni kwa shughuli za Bunge.