Dc Sima-Tutachukua hatua kwa Wakuu wa Shule watakaoweka Vikwazo kwa Watoto

GEORGE MARATO TV
0


 Angela Sebastian; Bukoba

Mkuu wa wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Erasto Sima amewataka walimu wakuu na wakuu wa shule za msingi na sekondari kutowawekea vikwazo wanafunzi wanaoripoti shuleni.

Aidha Sima amewataka wazazi kutotumia nafasi hiyo kushindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu ya shule ikiwemo sare,viatu na madaftari wakisingizia kusamehewa na Serikali.

"Tuwavumilie wanafunzi wanaoripoti kwa mara ya kwanza shuleni wa kidato cha kwanza,awali na darasa la kwanza wakati wazazi wakiendelea kuwaandalia mazingira rafiki ya kuendelea masomo"ameeleza DC

Pia amesema kuwa ofisi yake itahakikisha inafanya ufuatiliaji ndani ya wiki mbili ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaopaswa kwenda shule waende kwa asilimia 100.

Sima ameyasema hayo leo Januari 13,2025 wakati akitoa takwimu ya wanafunzi wanaopaswa kuanza kidato cha kwanza, darasa la kwanza na awali ambao tayari wamechukua fomu na wengine kujisajiri kwa ajili ya kuanza shule katika muhula wa kwanza kwa mwaka huu. 

Amesema asilimia 75 ya wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza mwaka huu walikuwa wameishachukua fomu katika halmashauri ya Bukoba ambapo wanafunzi 6,339 walishinda na kupangiwa shule mbalimbali hadi Januari 10,2025 wanafunzi 4,780 walikuwa wamechukua fomu sawa na asilimia 75 na Manispaa ya Bukoba waliopangiwa kwenda kidato cha kwanza wanafunzi 3,269 na waliokwisha chukua fomu wanafunzi 2,075 sawa na asilimia 63.4

Aidha amesema wazazi wanao uhuru wa kupeleka watoto shule za binafsi na kuwa wazazi watakaopeleka watoto wao katika shule hizo watoe taarifa kwa maafisa elimu ili watoto hao waweze kufuatiliwa kwa karibu.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top