Kamishna wa TRA Tanzania, Bw. Yusuf Juma Mwenda, afanya Mazungumzo na RC Sendiga

GEORGE MARATO TV
0

Leo tarehe 18 Desemba 2024, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, ameripoti katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, ambapo amepokelewa rasmi na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga.  

Katika ziara hii ya siku moja, Bw. Mwenda ameeleza kuwa lengo ni kukutana na wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara, kupitia hali ya ulipaji kodi, pamoja na kujadili fursa za ushiriki wa TRA katika miradi ya maendeleo ya kijamii (CSR). 


Aidha, Bw. Mwenda amepongeza juhudi za Mhe. Queen Cuthbert Sendiga kwa kuongoza mkoa ambao umekuwa na historia nzuri ya ulipaji wa kodi kwa mwaka 2024. Hili limekuwa chachu ya maendeleo ya mkoa wetu na taifa kwa ujumla.  

RC Sendiga amemuhakikishia Kamishna kuwa Mkoa utaendelea kuweka mazingira mazuri kwa TRA ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo sambamba na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wanapata elimu ya kodi na kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo endelevu ya mkoa na wananchi wake.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top