Tamasha la Bibi Titi Linafanya Kazi Nzuri ya Kuenzi Kazi za Serikali-Mhe. Mongella

GEORGE MARATO TV
0


Na John Jayros

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mhe. John Mongella amesema Tamasha la Bibi Titi  Mohamed siyo tu  Tamasha  linalotumika kumuenzi hayati  bibi Titi  bali ni Tamasha linalotumika kuenzi kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Mongella  ameyasema haya leo Desemba 13, 2024 wakati akifungua rasmi  tamasha la mwaka huu la Bibi Titi IKwiriri Wilayani Rufiji  huku akimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Mohamed Mchengerwa  kwa kazi  kubwa na nzuri anayoifanya  ya kuwaletea  maendeleo  wananchi wa jimbo  hilo.

“Ndugu wananchi wa jimbo la Rufiji, Sisi kama Chama  tunaliona jimbo hili ni miongoni mwa  majimbo salama  ambayo  yamefanya kazi nzuri kwa wananchi wake, hivyo mtambue  kuwa  mna  mbunge  bora”.Amefafanua  Mhe  Mongella

Ametoa  rai kwa  viongozi  wa CCM kote nchini kuendelea kushughulikia  kero za wananchi  na  kuachana na  kufikiria  ushindi  uliopita wa CCM badala yake  kuendelea kuwaletea  mandeleo

Kwa upande wake, Mhe Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais  kwa  kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya  ya Rufiji huku akimpongeza kwa maono  makubwa   na mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika  kipindi kifupi  cha uongozi wake.

“Naomba  kuchukua nafasi  hii kumshukuru Mhe. Rais kwa upendo wake kwa kuifanya  Wilaya ya Rufiji kuwa Mamlaka  ya Mji Mdogo hivyo kusaidia kunufaika na fedha za Benki ya Dunia” amefafanua Mhe. Mchengerwa 

Katika  ufunguzi  huo, Halimashauri ya Wilaya ya Rufiji imetiliana saini mkataba wa ujenzi wa  jengo la ofisi ya kisasa ya Wilaya  hiyo lenye  gharama ya zaidi ya Bilioni kumi.

Aidha,  Mhe.  Mchengerwa  ametumia  jukwaa hilo  kuwahakikishia  wananchi wa Rufiji  kuendelea  kutambua mchango wa hayati Bibi Titi na viongozi waliotangulia  na kwamba atashirikiana nao katika kuwaletea maendeleo ya kweli  

Amewashukuru umoja wa wanawake wa CCM kwa kuendelea kutambua  mchango wa Bibi  Titi na kuahidi kuendelea kuadhimisha  kila  mwaka.

Tamasha ya Bibi Titi Mohamed  la mwaka huu ni la nne na  limekuwa likiadhimishwa  kwa kuelezea  kazi kubwa inayofanywa na Serikali, ambapo  kesho linafikia kilele chake.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top