Profesa Kahyarara afungua Kongamano la Wahitimu NIT

GEORGE MARATO TV
0


Na Mwandishi Wetu, Dar

Katibu Mkuu wa wizara ya Uchukuzi Prof Godius Kahyarara amesema serikali inampango wa kutambua bunifu mbali mbali zinazofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu kikiwemo Chuo cha Taifa Cha Usafirishaaji na kuangalia namna ya kuzitumia kwa manufaa ya Taifa.

Ameyasema hayo leo jijini dar es salaam katika kongamano la 11 la wahitimu wa chuo cha Taifa cha usafarishaji NIT sambamba na kutoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika matokeo yao.

"Katika sekta ya usafirishaji tumeona ubunifu wa vifaa unaofanywa na wanafunzi na tumeviangalia kwa kuona namna gani vinaweza kusaidia katika sekta ya usafirishaji" amesema kahyarara

Ameongeza kuwa serikali imejipanga vizuri katika sekta ya usafirishaji na vitu vingi vimeongezeka ukiachana na mwanzo ilivyokuwa.

"Niwasahi vijana wanaomaliza vyuo vikuu kujipangana na kutambua kuwa kuna mda wakukomaa kabla ya kuingia kwenye soko la ajira na wasikate tamaa kwamba leo umemaliza shule na kesho ukupata ajira, kuna muda wa kujiandaa kabla.ya kuingia kwenye soko la ajira" amesema katibu mkuu

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Dkt. Prosper Mgaya amesema wanashukuru serikali ya Rais samia ambayo imekiwezesha chuo kujenga uwezo katika kutoa mafunzo kwa wataalam wa sekta ya usafirishaji.

"Tumepewa msaada wa kujenga miundombinu ya kujenga mabweni, madarasa kupitia mradi wa World Bank na kununua vifaa mbalimbali ambavyo tusingeweza kununua bila msaada wa serikali" amesema Lutangilo

Amengeza kuwa Chuo hicho kimewezeshawa na serikali na sasa kinatoa fani ya uandisi katika mafunzo ya reli, usafiri wa anga na mafunzo unafanisi wa meli huku vifaa vyote vya ufundishaji wamewezeshwa kutoka serikalini.

Naye Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambaye kwa sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Prof. Zacharia Mganilwa amesema kwa sasa wahitimu na wataalam mbalimbali hasa wale wa vyuo wapimane utendaji wao wa kazi kwa vitendo na sio kwa maneno na kuacha ile dhana ya kuogopana kwani kwa kupimana kufanya hivyo mipango mbalimbali ya serikali itafanikiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top