Ni waziri kijana myenyekevu na msikivu ambaye tayari ameweka rekodi ya kuhudumu Wizara nyingi kama Waziri hapa nchini
Mh Bashungwa huwezi mkuta anaropoka ropoka ovyo kwenye vyombo vya habari kufanya usanii katika majukumu yake,ni mtu anayeamini jambo na kulisimamia.
Mfano nzuri juzi juzi wakati mvua zimekata mawasiliano ya mikoa ya Kusini,waziri huyu wa ujenzi ambaye sasa anaenda mambo ya ndani alikesha kwa msiku na mchana kuhakikisha daraja la muda linajengwa na mawasiliano yanarejea,huyu si waziri wa kujitapa
Huwezi mkuta ana ugomvi na wenzie hata siku moja,ana heshimu mkubwa na mdogo
Lakini ndio Waziri anaonekana kupitia Wizara zote nyeti na zile zinazoonekana zinachangamoto. *Huu ni mfano mzuri kwetu kama Vijana kuishi maisha ya mh Bashungwa
Endelea kuwa na moyo huo katika kulitumikia taifa lako kwa kumsaidia mh Rais kila anapoona unastahili kumsaidia


Comments
Post a Comment