Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amefanya Uteuzi na Mabadiliko ya Viongozi mbalimbali akiwemo Profesa Palamaganda Kabudi ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mhe.Jerry Slaa ameteuliwa kuwa waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Wengine ni Mhe. Abdalah Ulega ameteuliwa kuwa waziri wa Ujenzi huku Mhe.Innocent Bashungwa akiteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka,Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa serikali, Kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa Kituo cha Kazi.
Aidha Profesa Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya afya na Tiba,Pamoja na Uteuzi huo Profesa Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili








.jpg)



Comments
Post a Comment