Baadhi ya wana CCM na wakereketwa wa chama hicho kata ya Nyasura wamempongeza kada wao Kambarage Wassira (Mmarekani)kwa kujitoa na kufanikisha ushindi mkubwa katika mtaa wa Zanzibar mjini Bunda mkoani Mara.
Wakizungumza na GMTV baada ya kumalizika uchaguzi wa Serikali za mitaa,baadhi ya wananchi hao wamedai juhudi kubwa za kada huyo zimewezesha ushindi wa CCM katika mtaa huo Bunda mjini.
Wamesema kulikuwa na figisu ambazo zilikuwa zikifanywa baadhi ya watu ndani na nje ya chama kwa kumpinga mgombea huyo mwana Mama Nyabaturi Ogola kitendo kilichomchukiza kada huyo na kuingilia kati kwa kupambana usiku na mchana hivyo kuwezesha ushindi huo wa CCM kwa kupata kura 586,huku Chadema ikipata kura 159 na NRA ikiambulia kura tatu
Wananchi hao wamesema wanatambua mchango wa ndugu Kambarage Wassira katika ushindi huo na kwamba wanakiomba chama Chao kiangalia namba ya kutoa tuzo kwa makada wanaojitoa katika kukipigania chama wakati wa kutafuta dola.