Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Viongozi wengine kwa ajili ya kumuombea aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Marehemu Dkt. Faustine Ndungulile aliyefariki dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu, wakati wa Kikao Kazi kilichofanyika Ikulu ndogo Arusha tarehe 29 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

Comments
Post a Comment