Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza anawatangazia wananchi wa Halmashauri hiyo waliojiandikisha kwenye Daftari la Makazi Kujitokeza kupiga kura kwenye Uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika Nchini Kote Novemba 27 Mwaka huu.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Missama,Zoezi la upigaji kura katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi litafanyika kwenye Vituo 736 Vilivyopo kwenye Vitongoji 723 pamoja na Vijiji 115.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Vituo vya kupigia kura vitakuwa wazi kuanzia saa mbili kamili za asubuhi na vitafungwa ifikapo saa kumi kamili za Jioni.
Aidha Makundi maalum ya wazee,akinamama wenye watoto wachanga, wajawazito na watu wenye ulemavu watapewa kipaumbele wakati wa zoezi la uchaguzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ina Jumla ya wapiga kura 267,260 ambao wanatarajiwa Kujitokeza kupiga kura kuwachagua Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji pamoja na Wajumbe wa Serikali za Vijiji.
Kauli mbiu ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa Mwaka huu ni Serikali za Mitaa,Sauti ya Wananchi,Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.

.jpg)
.jpeg)
.jpeg)
Comments
Post a Comment