Katika mangunzo hayo ambayo yamefanyika Ikulu ndogo Tunguru Zanzibar yamemhusisha pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda kwenye Kikao maalum cha maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) leo tarehe 12 Novemba, 2024.





