Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Chamapinduzi(CCM)Taifa LEONARD QWIHAYA Maarufu kwa Jina la Manguzo ametangaza ajira Mia mbili za udreva wa Magari Makubwa.
Kwa mujibu wa Tangazo la ajira lilitolewa na Kampuni ya QWIHAYA GENERAL ENTERPRISES COMPANY LTD inayomilikiwa na MNEC huyo,imeeleza kuwa Mchakato wa Maombi ya ajira ni bure na waombaji wasikubali kuhadaiwa na Matapeli.
"Nachukua fursa hii kuwatangazia Watanzania wenzangu kuwa, kupitia Kampuni yetu ya Qwihaya tumetangaza fursa za Ajira kwa Maafisa Usafirishaji (Dreva) 200 wa Magari Makubwa ya Mizigo,Kutokana na maombi maalum kwa Wakazi wa Mkoa wa Mwanza tumeweka utaratibu rafiki kwa ambao hawana wadhamini wa serikali hivyo, wataambatanisha barua tatu za wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi ikiwemo uthibitisho wa Balozi wa Shina analotoka, kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Tawi pamoja na Kata"Manguzo ameeleza katika Taarifa yake.
Kwa Mujibu wa Manguzo,Dhamira ya Kampuni yake ya QWIHAYA GENERAL INTEPRISES COMPANY LTD ni kuwekeza uwekezaji unaunganisha mnyororo wa thamani ikiwemo fursa ya ajira kwa Vijana.
Aidha amemshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema kuendelea kumpa nafasi ya kuwatumikia Watanzania na nashukrani za pekee ni kwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Jemedari Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutuwekea mazingira rafiki ya uwekezaji nchini Tanzania.



