Biden na Trump Kukutana Jumatano Wiki hii

GEORGE MARATO TV
0


 Bideni na Trump watakutana Jumatano Hii na kuzungumza maswala Mbali Mbali kuhusu Nchi na Kuachiana Madaraka kutoka Utawala wa Biden kwenda Trump

Ikumbukwe kumekua kuna Shutuma Nyingi Sana kutoka kwa Trump kwenda kwa Utawala wa Biden Ambao amekuwa akijaribu kutoa Shutuma na hoja nyingi kwamba Biden Ameshindwa kushughulikia maswala mbali mbali ya kiuchumi na Sera ya Mambo ya Nje pamoja na Uhamiaji ambazo Zimekuwa ni Sera za Msingi kwa Trump ambapo imepelekea Nchi kwenda Mrama

Hiki kinachoenda kutokea Kesho kutwa Dunia Nzima itakuwa ina Subiri kwa hamu kubwa kuona ni namna gani Viongozi hawa Wenye Ushindani mkubwa watakavyozungumza

Tukumbuke kwamba Trump amekuwa akiweka maoni yake wazi ya kihafidhina na kitaifa zaidi pale ambapo anapozungumzia maswala ya kitaifa Zaidi

Kuna Vitu vinawatofautisha Viongozi wa Marekani katika falsafa ,Mitazamo,Sera na Vipaumbele lakini kuna vitu vinawaunganisha ambayo ni maslahi ya Taifa lao kwa Kiasi kikubwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top