Na Angela Sebastian-Bukoba
Jitihada za waandishi wa habari za kupinga ukatili wa kijinsia zimezaa matunda mtuhumiwa wa ubakaji akamatwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amethibitisha kukamatwa kwa mwalimu wa taaluma Lameck Jonas wa shule ya msingi Rulanda kata ya Rulanda wilaya ya Muleba mkoani humo ambaye anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake muhitimu wa darasa la saba (13)
Akiongea kwa njia ya simu kamanda Chatanda,amesema kwa jitihada za jeshi hilo wamefanya msako na kufanikiwa kumkamata na sasa yuko mikononi mwa jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Kamanda Chatanda,anasema taratibu nyingine za kisheria zinaendelea na muda wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 30, mwaka huu majira ya jioni baada ya mtoto huyo akiwa na wanafunzi wenzake kufika shuleni hapo majira ya mchana kwa ajili ya kuomba mwalimu huyu awaangalizie matokeo ya mtihani wa darasa la saba, ndipo alimwambia aliyefanyiwa ukatili kuwa ameshindwa mtihani hivyo arudi baadaye ili ampe ushauri.
Ukatili huo wa mtoto huyo uliibuliwa na chama cha waaandishi wa habari wanawake mkoa wa Kagera (JWK) wanaopinga ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto
Novemba 4 mwaka huu, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi ambao wameendelea kukerwa na vitendo hivyo vinavyoendelea kuleta hofu katika jamii.
