WANANCHI wa vitongoji elfu 20,000 kati ya 31,0000 ambavyo havijapata nishati ya umeme hapa nchini wanatarajia kunufaika na programu maalum ya kuwezeshwa huduma ya hutumia nishati safi yq kupikia,kupitia wakala wa nishati vijijini (REA), ambapo itasaidia kuchechemua shughuli za maendeleo.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu wa REA, mhandisi Hassan Said katika kikao cha pili cha mwaka cha wadau wa maendeleo ya nishati vijijini kilicholenga kufanya tathimini ya mipango ya utekelezaji wa miradi kwa mwaka huu wa fedha.
Kikao hicho kimefanyika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo Mhandisi Said amesema program hiyo imetokana na ubunifu wa Rais Samia Suluhu Hassan amba yeye anatamkwa kuwa kinara wa kampeni ya nishati safi hivyo Serikali yake na wafadhiri mbalimbali wamewezesha kufikia vitongoji 20,000.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amewahakikishia wadau wa maendeleo ya nishati kuwa fedha zinazotolewa zitaendelea kutukika kwa usahihi na uwepo wa umeme wa uhakika kwenye baadhi ya maeneo ya mkoa huo wananchi wamejiongezea kipato kwa kutumia nishati.

