Kamati ya amani ya viongozi wa dini mwanza yataka uchaguzi huru na haki na wenye kuaminika

GEORGE MARATO TV
0



Wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani mwanza wametakiwa kutenda haki katika hatua zote za uchaguzi huo ikiwemo uteuzi wa wagombea pamoja na kutangaza matokeo. 

Wito huo umetolewa na mwenyekiti mwenza wa kamati ya amani ya viongozi wa dini mkoani humo Sheikh Hassan Kabeke wakati wa kongamano la kuhamasisha ushiriki wa wananchi wa magu Katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 


"Wasimamizi wa uchaguzi tendeni haki katika uchaguzi huu, muhakikishe mnatangaza washindi halali,hii ni muhimu katika kuwezesha kutamalaki kwa amani na utulivu" alisema Sheikh Kabeke

Aidha amewasihi wagombea watakaoshindwa kwenye  uchaguzi wa serikali za mitaa kukubali matokeo ili kuepusha vurugu. 



Naye Askofu Dokta Robert Bundala ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya amani ya viongozi wa dini mkoani mwanza amehimiza suala la uzalendo miongoni mwa watanzania



Ametaka uzalendo kwa taifa utakuwa na maana ikiwa watu wote waliojiandikisha watajitokeza kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 

"Wagombea wanapaswa kujenga hoja wakati wa kampeni na si matusi ili kuepusha uvunjifu wa amani" alisema Askofu Sekelwa

Kongamano hilo lililoshirikisha makundi mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya vijana na wanawake limeandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini. 





Mkurugenzi wa shirika hilo Yassin Ally amezungumzia umuhimu wa wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 



Yassin amehimiza wananchi wasikilize Sera za wagombea wakati wa kampeni ili kuchagua viongozi Bora. 

"Mjiepushe kuchagua kwa mihemko na badala yake mzingatie Sera zitakazowaletea maendeleo badala ya kuchagua kwa misingi ya vyama,itikadi,ukabila na UgandaUganda pamoja na rushwa" alisema Yassin

Akizungumza katika kongamano hilo,Mkuu wa wilaya Magu Joshua Nasari amewahakikishia usalama wananchi wakati wote wa uchaguzi na kuwaasa wananchi kuwa walinzi wa amani kabla,wakati na baada ya uchaguzi huo





Nasari pia amewahakikishia wadau wa uchaguzi pamoja na wananchi kuwa serikali imedhamiria kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na wenye kuaminika.

Uchaguzi wa serikali za mitaa umepangwa kufanyika novemba 27 mwaka huu ambapo zaidi ya wapiga kura laki mbili wilayani magu wanatarajiwa kuchagua wenyeviti wa vitongoji,vijiji na mitaa pamoja na wajumbe wa serikali za mitaa na vijiji. 













Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top