Shule ya Sekondari Ruhinda Waiomba REA Kusaidia Kupata Nishati Safi ya Kupikia

GEORGE MARATO TV
0

 


Na Angela Sebastian Karagwe

WATUMISHI na wanafunzi wa shule ya sekondari jumuishi ya Ruhinda iliyopo kata ya Nyaishozi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia huduma ya Nishati ya umeme kupitia wakala wa Nishati vijijini (REA) pia wameomba kuwaboreshewa miundombinu ya Nishati ya kupikia inayotumiwa na wapishi shuleni hapo kwasasa ni hatari kwa afya zao.

Walitoa ombi hilo jana wakati  bodi ya  REA ikiongozwa na mwenyekiti wake balozi meja jenerali mstaafu Jacob Kingu ilipofanya ziara shuleni hapo kwa lengo la kujionea maendeleo ya miradi ya REA vitongojini inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, ambapo shule hiyo ni miongoni mwa wanufaika.

Katika taarifa ya mkuu wa shule hiyo Ambrose Katorogo na shairi kwa niaba ya wanafunzi lililoimbwa na mwanafunzi mwenye uoni hafifu Asifiwe Erasto walisema kuwa kupitia Nishati ya kuni wanayotumia wapishi wa shule hiyo kwa sasa inawaathiri kiafya.

Mwalimu Katorogo ameongeza  kusema, wao wanatamani kutumia Nishati ambayo ni rafiki wa Mazingira ili kwendana na Sera ya Serikali ya kutunza  mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi

"Tunaishukuru Serikali ya hawamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta huduma za umeme huku vijijini ikiwemo shule yetu ambapo tumeweza kupata manufaa makubwa kama vile kuokoa zaidi ya shilingi 430,000 kwa mwezi ambayo ilikuwa ikitumika kuchapisha mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wetu na sasa tunatumia gharama isiyozidi  sh. laki moja"ameeleza mkuu wa shule 

Naye Mwenyekiti wa bodi ya REA  balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amasema  kuwa suala hilo la matumizi ya Nishati shuleni hapo litapata mwarobaini ili kuhakikisha wanatumia Nishati safi hivyo likifikishwa kwenye bodi halitakwama kwasababu wao wanaunga mkono kampeni ya Rais Samia  ya kuhakikisha wanachama wote wanatumia nishati safi  ya kupikia.

Aidha mkurugenzi mkuu wa REA mhandisi Hassan Saidy anasema pale palipo na giza panahitajika kuongezewa  umeme hilo ni jukumu lao kuhakikisha linafanikiwa pia kwa suala la nishati ya kupikia katika shule hiyo wanaendelea kulifanyia tathimini kwa kuweka mifumo ya gesi safi itakayo faa zaidi na mfumo wa jiko banifu la kisasa ambalo hutumia kuni na mkaa kwa usalama zaidi.

Naye mkurugenzi wa umeme vijijini kutoka REA Jones Olotu anasema kuwa  vitongoji 3,765 vya mkoa wa Kagera vinatarajiwa kunufaika na nishati ya umeme wa REA ambapo vitongoji 1887 kati ya hivyo tayali vimepata umeme  kutokana na mpango wa Serikali wa kuhakikisha umeme unafika kila kona.

Naye Asifiwe Erasto ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza shuleni hapo anasema kupatikana kwa nishati ya umeme shuleni hapo imeongeza na kuimalisha usalama hususani kwa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali ikwemo wenye uoni hafifi na wenye ualbino wakati wa usiku na wengine wanaweza kujisomea kutokana na uwepo wa mwanga wa kutosha.

Shule ya Ruhinda inao wanafunzi wapatao 775 ambapo kati ya hao 75 ni wenye mahitaji maalum.

Katika ziara ya Mwenyekiti wa bodi ya REA kwenye wilaya ya Karagwe  pia walitembelea mradi wa maji uliounganishiwa huduma ya umeme na REA kwa ajili ya kusukuma maji uliopo katika kata ya Kituntu.




Picha ya Mwanafunzi Asifiwe Erasto kidato cha kwanza mwenye uoni hafifu anayesoma katika shule Jumuishi ya Ruhinda Sekondari Wilayani Karagwe akisoma risala  mbele ya bodi ya REA .




Bodi ya REA na walimu wa shule ya Sekondari Ruhinda Wilayani Karagwe mkoani Kagera katika picha ya pamoja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top