* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Tamasha hilo litafanyika kuanzia novemba sita hadi kumi mwaka huu mjini shirati.
Ofisi ya Mkuu wa wilaya Rorya inakaribisha wananchi wote pamoja wadau mbalimbali kushiriki kwenye tamasha hilo litakalozinduliwa na Mkuu wa wilaya hiyo Dokta Khalfan Haule.
Miongoni mwa matukio muhimu yatakayopamba Tamasha la Rorya fursa festival ni pamoja na fursa za kilimo,uvuvi,ufugaji,michezo na utalii pamoja na mbuzi,kondoo,samaki na nyama choma.
Tamasha hilo litahimitishwa na mashindano ya mbio za mitumbwi katika eneo la mwalo wa sota,mashindano ya kuchoma nyama,maonesho ya fursa pamoja na kutoa vyeti kwa wawekezaji,wajasiriamali pamoja na idara zote wilayani Rorya.
Kauli mbiu ya Tamasha hilo ni Rorya na Uwekezaji endelevu kwa uchumi wa viwanda