NAIBU Waziri Mkuu na waziri wa Nishati Mh Dkt Dotto Biteko kuongoza Maafisa Jenerali, Maafisa Wakuu, Maafisa wadogo na Askari wa JWTZ kuaga mwili wa mkuu wa majeshi mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri.
Mh Biteko atamwakilisha amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania mh Dkt Samia Suluhu Hassan kuaga mwili huo novemba 01- 2024 katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika saa tatu asubuhi kabla ya mwili huo kusafirishwa kuelekea Butiama mkoani Mara kwa ajili ya shughuli ya mazishi.
Jenerali Musuguri alifariki dunia asubuhi ya Oktoba 29 mwaka 2024 wakati akapatiwa matibabu hospitali ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza,enzi za uhai wake ameshika nafasi mbalimbali ndani ya jeshi hadi kuwa mkuu wa majeshi kuanzia mwaka 1980 hadi 1988 alipostaafu kwa heshima.
Jenerali Musuguri akiwa jeshini amekuwa mkufunzi wa askari wakati wa ukoloni wa Mwingereza. Mwaka 1953 alimfundisha pia Idd Amin katika kambi ya mafunzo ya Kahawa Barracks nchini Kenya.
Hivyo mwaka 1978 katika vita vya Kagera, Mwalimu aliingia vitani na Mwanafunzi wake na akamshinda!
