Jeshi la polisi mkoani mwanza linamshikilia Amos Mwita Mkazi wa Bugarika bendera tatu,wilayani nyamagana kwa tuhuma za mauaji ya Daniel Kisire Mkazi wa bugarika sokoni.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa Mwita anatuhumiwa kutenda mauaji hayo kwa kumchoma Kisire na Kitu chenye ncha kali shingoni baada ya kuzuka kwa ugomvi uliozuka uliotokana na wivu wa kimapenzi na kusababisha kifo chake.
Kamanda Mutafungwa amesema kuwa mara ya baada ya mtuhumiwa Mwita kufanya tukio hilo alitoroka na kwenda kusikojulikana ambapo Jeshi la polisi lilifanikiwa kumtia mbaroni akiwa mafichoni nyumbani kwa rafiki yake katika eneo la bugarika.
"Daniel Kisire ambaye ni marehemu na Amos Mwita ambaye ni mtuhumiwa walikuwa wanaishi Jirani katika eneo la bugarika ambapo marehemu alimtaka kimapenzi binti mmoja ambaye alimkatalia na baadaye binti huyo alianza mahusiano na Mwita na huo ndo ukawa chanzo cha ugomvi baina ya marehemu na mtuhumiwa"alisema kamanda mutafungwa
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ambapo Jeshi la polisi limetoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepusha kutokea kwa matukio yanayoweza kuzuilika.
