Waziri mkuu Majaliwa kufungua kongamano la kujadili bima ya afya kwa wote Jijini Arusha

GEORGE MARATO TV
0


TANZANIA imeitisha kongamano kubwa kwa ajili ya kujadili Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, sambamba na Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Mpango wa Ufadhili wa Sekta ya Afya kwa kuhusisha wataalam wa sekta ya afya wa ndani na nje ya nchi.

Kongamano hilo na mdahalo huo wa kitaifa unatarajia kufunguliwa na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa oktoba 30 katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha jijini Arusha.

Tayari wadau hao wa sekta ya afya wameanza kongamano lao leo  tarehe 29 na kutegejea kumalizika kwa matukio hayo mawili 01 Novemba 2024.

 Wataalamu hao kutoka sekta mbalimbali wa ndani na nje ya nchi watajadili mikakati inayofaa kutumiwa na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuboresha huduma za afya kwa wote.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na wabia wa maendeleo imeshiriki uratibu wa maandalizi ya matukio hayo muhimu ambapo Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Mpango wa Ufadhili wa Sekta ya Afya, kufanyika kwake ni utekelezaji wa maagizo ya Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa kikao chao kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Mei 2024. 

Aidha, mdahalo huo ni utekelezaji wa maazimio ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika waliyoyatoa katika Mkutano wao uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia Julai 2019.

Katika siku yake ya kwanza, washiriki wa kongamano hilo walipata fursa ya kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na watalaam wa afya. Kabla ya mada hizo kuanza kuwasilishwa, zilitanguliwa na hotuba fupi kutoka kwa Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu na Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Afya, Bw. Amoury A. Amoury. 

Watalaamu hao waliwambia washiriki madhumuni ya kongamano hilo na matokeo yanayotarajiwa na dira ya mpango wa bima ya afya kwa wote nchini Tanzania.

Mada nyingine zilizowasilishwa katika siku ya kwanza ni pamoja na  Kugharamia Mfumo wa Afya kwa Wote: Kuangalia kwa kina mikakati ya kibunifu kwa ajili ya Upatikanaji Endelevu wa Fedha; (Financing Universal Health: Exploring Innovative Strategies for Sustainable Funding in Tanzania); Nafasi ya Teknolojia na Ubunifu katika Kuboresha Ufanisi na Upatikanaji wa Huduma ya Bima ya Afya kwa Wote; (Role of Technology and Innovation in Improving Access and Efficiency in Universal Health Insurance); na Enrolment and Re-enrolment Strategies - what works and what does not work.

Wizara inawakilishwa na timu ya watalaamu katika kongamano hilo inayoongozwa na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Mhandisi Abdillah Mataka na siku ya ufunguzi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Denis Londo (Mb) atashiriki hafla ya ufunguzi ya matukio hayo.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top