Mbunge wa Njombe Mjini Mhe.Deo Mwanyika amewahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura , zoezi litakalohitimishwa Oktoba 20, 2024.
Ameyasema hayo Oktoba 19, 2024 wakati akijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika Mtaa wa Uwemba.
Amesisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi kwa kuchagua viongozi katika mitaa na vijiji.
Ameongeza kuwa kujiandikisha ni muhimu lakini kushiriki kupiga kura ni muhimu zaidi kwani mwananchi unakwenda kuchagua kiongozi unayemtaka kwa ajili ya maendeleo ya mitaa na vijiji vyetu.
*Serikali za mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze kushiriki uchaguzi*