Waziri anusuru maelfu ya abiria na magari yaliyokwama baada ya barabara kufungwa

GEORGE MARATO TV
0



Wananchi wa kijiji cha Magubike wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro wamefunga barabara kuu ya Dodoma-Morogoro kwa zaidi ya saa Saba baada ya mtoto Nuru anayesoma elimu ya awali kugongwa na gari inayodaiwa kuwa ya serikali.

Kufungwa kwa barabara hiyo kuu ya Morogoro -Dodoma kumesabisha msururi mkubwa wa magari  yakiwemo mabasi ya abiria

Uamuzi wa kufunga barabara hiyo umechukuliwa na wananchi ili kushinikiza serikali kuweka matuta kwenye eneo hilo ili kupunguza ajali zinazotokea Mara kwa Mara na kukatisha uhai wa baadhi ya watu na kujeruhi wengine. 

 Mwenyekiti wa kijiji cha Magubike Salum Chapa wamesema kwa kipindi kifupi tayari watu tisa wamegongwa katika eneo hilo na hakuna hatua ambazo zimechukuliwa



Miongoni wa watu waliokwama kufuatia kufungwa kwa barabara hiyo ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Seleman Jafo na Msafara wake. 

Akiwa katika eneo hilo,Dkt.Jafo alilazimika kuzungumza kwa njia ya siku na Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa ambaye ameahidi wakala wa barabara nchini(Tanroads) katika kwenye eneo hilo na kuweka matuta.

Akizungumza na wananchi hao,Jafo amewaomba kuwa na subra jambo hilo ameliona na amewasiliana na waziri Bashungwa na hatua za haraka zitachukuliwa  kama wananchi wanavyotaka

Ahadi ya kuwekwa matuta ilileta matumaini kwa wananchi wa kijiji cha Magubike ambao waliruhusu magari kwanza kupita ambapo wanajeshi waliokuwa eneo hilo waliweza kusimamia na kuruhuru magari kuanza kupita ikiwa ni saa 1.45 asbh Oktoba 19








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top