Mwili wa Mbuge wazikwa kijeshi kwa kupigwa mizinga kumi na mitatu

GEORGE MARATO TV
0


Hatimaye Mwili wa meja Jenerali mstaafu wa jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania Chalres Mbuge umezikwa kwa heshima zote za kijeshi kijijini kwake.

Mwili  wa afisa huyo wa ngazi ya juu wa JWTZ  umezikwa leo Oktoba 17 2024 majira ya saa sita na dakika 13 katika kitongoji cha Nyamongo,kijiji cha Kiabakari wilayani Butiama mkoani Mara.

Mazishi hayo yaliongozwa na kanisa katoliki kabla ya kufanyika kijeshi yameshuhudiwa na mkuu wa majeshi mstaafu jenerali VENACE MABEYO,wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu wakiongozwa na mkuubwa mkoa wa Mara kanali Evans Mtambi.




Maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la wananchi wameongozwa mkuu wa jeshi la kujenga  Taifa (JKT)  meje jenerali Rajab Mabele akimwakilisha mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini jenerali JACOBO JOHN MKUNDA. 

Akizungumza kabla ya mazishi hayo,meja Jenerali Mabele mbali na kumuelezea marehemu enzi za uhai wake jinsi alivyokuwa mshauri katika majukumu mbali mbali ya kikazi amesema Taifa limepata pigo kwa kulndokewa na meja Jenerali Mbuge kwa vile mchango wake bado ulikuwa ukihitajika.

Amesema mkuu wa majeshi amesikitishwa mno na kifo hicho kwa kusema kuwa enzi za uhai wake alilitimikia Taifa kwa heshima kubwa hasa katika kusimamia kikamilifu majukumu yote aliyokabidhiwa.

Kwa sababu hiyo jenerali Mkunda ameitaka familia na Watanzania kuiga mfano huo wa utumishi kwa kukubali kufanya kazi kwa bidii na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake mkuu wa majeshi mstaafu jenerali Venance Mabeyo,amesema alimfamu vema marehemu kwa vile alikuwa mmoja ya walimu wake katika mafunzo ya kijeshi na kwamba amelitumikia taifa kwa heshima kubwa.

Hata hivyo jenerali Mabeyo ameiomba familia kushikamana sasa kuliko wakati wowote na kuwa kitu kimoja katika kumuenzi meja Jenerali Mbuge.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mara kanali Mtambi akizungumza katika mazishi hayo,mbali na kuelezea mchango wa marehemu Mbuge enzi za uhai wake,amesema Watanzania wana kila sababu kulitumikia taifa hili kwa upendo na kwamba inapotokea umeitwa na mwenyezi Mungu uweze kuwa na historia njema ya kusimuliwa.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka Wana Mara kushikamana pia kujitokeza kujiandikisha katika daftari la makazi.

Katika mazishi hayo ya kijeshi,maafisa wa cheo cha meja waliubeba mwili wa marehemu huku wakisindikizwa na maafisa wa cheo cha kanali kisha kuuweka juu ya kaburi.



Baada ya maafisa hao kuweka mwili juu ya kaburi,maafisa wa cheo cha kanali walifanya kazi ya kuushusha kaburini kisha ishara za mazishi zilifanyika na kufuatiwa na upigaji wa mizinga kumi na tatu.

Katika mazishi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na mkuu wa utumishi jeshini meja Jenerali Michael Gagati baadhi ya wananchi wameoneshwa kusikitishwa na kifo hicho kwa kuelezea kuwa enzi za uhai wake mzee meja Jenerali mbuge alishirikiana vema na jamii hiyo.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top