Comoro yatafuta fursa za ushirikiano na miji ya Tanzania

GEORGE MARATO TV
0


Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu,amekutana na Rais wa Umoja wa Mameya Nchini Comoro,Nassuf Ahmed Abdallah ambaye amemueleza kuwa wangependa kuona ushirikiano wa miji ya Comoro na Tanzania.

Mheshimiwa Abdallah ambaye pia Meya wa Mji wa Domoni uliopo katika Kisiwa cha Anjouan amesema ushirikiano huo wa miji ya Comoro na Tanzania utafungua fursa za kiuchumi kwa kuwa tayari kuna uhusiano mkubwa wa kijamii na kihistoria baina ya raia wa nchi hizo mbili na kuongeza kuwa kwa upande wa Domoni wangependa kuwa na ushirikiano na Manispaa ya Mji wa Mtwara ambao tayari wamewahi kufanya ziara huko siku za nyuma.

Kwa upande wake,Balozi Yakubu alimhakikishia kuwa ombi hilo atalifikisha Tanzania ili lifanyiwe kazi na kusifu ushirikiano anaoupata kutoka kwa Mameya wa Miji mbali mbali anapoitembelea na kuongeza kuwa uhusiano wa miji utasaidia pia kuongeza ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya nchi hizo mbili.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top