Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe Esther Matiko ameendelea na ziara yake ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kufika Shule ya Sekondari Tagota na kuzungumza na Walimu na Wanafunzi wa Shule hiyo.
Akiwa Shuleni hapo kupitia taasisi ya Matiko Foundation,Mhe Esther Matiko amekabidhi Tank la Maji Lita 5,000 lenye thamani ya Tsh 1,350,000/= kwa ajili ya uvunaji wa maji yatakayotumiwa na Walimu na Wanafunzi wa Shule hiyo.
Mhe Esther Matiko ameweza pia kutoa vifaa vya michezo kwa wanafunzi wa Shule hiyo kupitia taasisi ya Matiko Foundation ambavyo ni Mipira Pete na Mguu na Jezi Mpira wa Pete na Miguu vyenye thamani ya Tsh 850,000/=
Akipokea changamoto za Walimu shuleni hapo kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Shule Mwl Nulu Mwalukasa be amemueleza Mhe Matiko Shule hiyo haina jengo la utawala jambo ambalo linaleta usumbufu kwa walimu.
Mhe Esther Matiko ameahidi kwenda kuliwakilisha bungeni suala hilo kwani ukosefu wa jengo la utawala limeonekana kuwa changamoto kubwa kwa Shule za Wilaya ya Tarime.
Walimu na wanafunzi wa Shule hiyo wamempongeza Mhe Esther Matiko kwa kujitoa kwake kuhakikisha maendeleo ya elimu yanasongambele.