Waziri Bashe Azindua Kiwanda Cha Kubangua Korosho Mtwara

GEORGE MARATO TV
0



Na Elizabeth Cornely

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amezindua kiwanda cha kubangua korosho Newala mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa Bashe, kiwanda hicho kimegharimu Sh.bilioni 3.4.

Chama Kikuu cha Ushirikia cha TANECU  kimeanza safari ya kuwa na ushirikia imara kwa kujenga kiwanda cha kubangua korosho Newala, mkoani Mtwara.

Bashe ambaye yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi, amekipongeza TANECU kwa kuwa mfano mzuri wa kuonesha ushirika unaozidi kuwa imara kwa kuhakikisha uwekezaji huo wa kiwanda ni wa wakulima wenyewe. 

Pia, alielekeza kijengwe kiwanda kingine kama hicho Tandahimba na kiwe tayari msimu ujao.

Kiwanda hicho cha kubangua korosho kilichozinduliwa, kina uwezo wa kubangua tani 3,500 kwa mwaka na kwamba mkakati ni kuwa na viwanda 20 vya Kubangua Korosho chini ya TANECU katika Mkoa wa Mtwara ambapo 10 vitajengwa Newala na 10 vingine vitajengwa Tandahimba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top