Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony MAVUNDE ametimiza ahadi yake ya kuwapatia Vijana wa Hamasa wa Chama Chamapindizi(CCM)Dodoma Mjini vifaa ikiwemo seti moja ya Matarumbeta na Ngoma kwa ajili ya kuchagiza shughuli mbalimbali.
Akikabidhi vifaa hivyo,Mavunde ambaye pia ni Waziri wa Madini amewaasa vijana hao kuvitumia vifaa vilivyotolewa kama kitega uchumi cha kujiongezea mapato kupitia sherehe mbalimbali.
Matarumbeta na Ngoma yamegharimu shilingi millioni mbili na nusu huku Mavunde akiahidi Kuongeza seti nyingine mbili ili kuboresha huduma inayotolewa na vijana hao kwenye sherehe mbalimbali.
Mbali na Matarumbeta na Ngoma,Mavunde pia amewapatia vijana wa Hamasa(CCM)Dodoma Mjini mashine ya kufyatua matofali yenye thamani ya shilingi millioni kumi.
Kwa upande wake,Uongozi wa Vijana wa Hamasa(CCM)Dodoma Mjini wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa kutimiza ahadi yake kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ya kujiongezea kipato.