Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo ameshiriki kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mafunzo kwa Wajumbe wa Baraza Kuu. Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Mohammed Ali Mohammed (Kawaida), kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), jijini Dodoma, leo Septemba 17, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.




Comments
Post a Comment