MCHUNGAJI wa Kanisa la Uzima Tele Mtume Samuel Kisinza ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake inazofanya kwenye sekta mbalimbali hapa nchini ambazo zinachochea ukuaji wa uchumi.
Alisema hayo Jana katika Ibada ya Jumapili kwenye Kanisa hilo Nundu Jijini Mwanza ambapo alipongeza kuanza kwa safari za Reli ya Kisasa (SGR),kuanza kwa uzalishaji Umeme kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere, kukaribia kukamilika kwa daraja la Kigongo Busisi na kukamilika kwa Miradi ya kimkakati katika Mikoa mbalimbali.
Mtume Kisinza amesema jitihada hizo zimedhihirika katika maeneo ya sekta za kilimo,uvuvi,mifugo,usafirishaji,elimu,Afya ambapo mikoa yote hapa nchini imeguswa na kazi za Serikali ya Awamu ya Sita.
Alisema vilevile kuwepo kwa usitahimilivu wa kijamii hapa nchini nayo ni njia mojawapo mhimu kwa Ujenzi wa uchumi unaofanywa na Serikali hii.