Na Shomari Binda-Musoma
MKURUGENZI wa Le Grand Victoria Hotel ya mjini Musoma Rama Msomi Bwana amewashauri washiriki wa shindano la Miss Lake Zone kuwa wabunifu na kuutagaza utalii wa ndani.
Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake na meneja wa hotel hiyo Paul Mutinda alipokuwa akizungumnza nao kwenye kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika ukumbi wa Le Grand Beach.
Amesema urembo ni fani na inahitaji ubunifu kama zilivyo fani nyingine ili kuwafanya kuwa juu zaidi na kujitangaza.
Mkurugenzi huyo amesema warembo ndio wanaotangaza masuala ya utalii na wakiweka ubunifu wataifanya kazi yao vizuri.
Amesema wapo waliofanya fani ya urembo na wamefanikiwa kufika mbali na kuwataka washiriki wa miss lake zone kujitambua na kuwa na tabia njema.
Mkoa wa Mara na kanda ya ziwa ni kitovu cha utalii hivyo mkurugenzi anawashauri kuwa mabalozi wa masuala ya utalii"Amesema.
Kwa upande wao washiriki wa shindano la Miss Lake Zone wamesema wamezunguka mkoa wa Mara kwa siku 4 wameona fursa zilizopo na wanakwenda kuwa mabalozi wazuri.
Wamesema ushauri waliopata kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara waliyozunguka wanakwenda kuufanyia kazi