Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amembelea kiwanda na kituo cha utafiti kinachotengeneza Viatilifu na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba, Agosti 13, 2024. Kulia kwake ni rais wa kiwanda na kituo hicho Rod Manuel Valdes. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara maalum ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Cuba.
Tazama habari picha za matukio mbalimbali
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rodi Manuel Valdes ambaye ni rais wa Kiwanda na Kituo cha Utafiti kinachotengeneza Viatilifu na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba alipokitembelea, Agosti 13, 2024. Mheshimiwa waziri Mkuu alikuwa katika ziara maalum ya kuboresha mahusiano kati ya Cuba na Tanzania.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kiwanda na Kituo cha Utafiti kinachotengeneza Viatilifua na Viuadudu cha Labiofam kilichopo Boyeros nchini Cuba alipokitembelea, Agosti 13, 2024. Wa tatu kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, wa pili kulia ni Rais wa kiwanda hicho Rodi Manuel Valdes na kushoto ni Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Yordenis Despaigne Vera. Mheshimiwa waziri Mkuu alikuwa katika ziara maalum yakuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Cuba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Rais wa Kiwanda na Kituo cha Utafiti cha Biocuba Farm cha nchini Cuba Bi. Mayda Mary’s baada ya kutembelea kiwanda na kituo hicho kinachotengeneza chanjo za magonjwa mablimbali, Agosti 13, 2024.
*Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


.jpg)

Comments
Post a Comment