William Mabusi – WyKS Butiama*
Mbunge wa Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amewaahidi wananchi wa Kata ya Busegwe kuwa watapatiwa maji kutoka Mradi mkubwa wa maji wa Mgango, Kiabakari na Butiama kama sera ya maji inavyosema.
Mhe. Sagini ameyasema hayo kwenye Mikutano wa hadhara aliyoifanya kwa nyakati tofauti kwenye Vijiji vya Nyanza, Busegwe na Kigori Kata ya Busegwe, Agosti 11, 2024.
“Mradi wa maji wa Mgango, Kiabakari hadi Butiama umeshafika kijiji cha Bumangi, kinachotakiwa kufanyika ni usambazaji wa maji kwenye vijiji vinavyozunguka bomba kubwa la mradi huo kwa kipenyo cha kilomita 25, yaani vijiji vilivyo umbali wa kilomita kumi na mbili na nusu upande mmoja wa bomba na kilomita kumi na mbili na nusu upande mwingine.” Alisema.
Akiongelea uhitaji wa umeme kwa wananchi wa Kata hiyo Diwani wa Kata ya Busegwe Mhe. Hesha Kisibo amesema jumla ya vitongoji kumi na nne vya Kata yake ni vinne tu vimepata umeme na kwa kuwa katika Mpango wa TANESCO Mkoa wa Mara kwa mwaka 2024/25 wa usambazaji umeme kwa Wilaya ya Butiama, Kata ya Busegwe iko kwenye Mpango huo, Diwani huyo amemwomba Mhe. Sagini kuunganisha nguvu ili vitongoji zaidi vya Kata hiyo vipate umeme.


.jpg)
.jpg)
Comments
Post a Comment