WANANCHI wa waishio kisiwa cha Rukuba kilichopo jimbo la Musoma vijijini wamefurahia kupata mradi wa umeme jua( Solal Energy) ambao wamesema utasaidia kupunguza Changamoto wa upatikanaji wa Nishati hiyo.
Wakizungumza kwa njia ya simu na George Marato TV wamesema mradi huo umekuja kuondoa changamoto nyingi kwao kutokana na Kuishi kisiwani.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Rajabu Msweta amesema wamekuwa hawapati huduma za uhakika za umeme kutokana na kuwa kisiwani.
Amesema serikali kupitia Tanesco wanawapelekea mradi wa umemejua ambao wanaamini utakuwa suluhisho la matatizo.
Rajabu amesema umeme ni uhitaji mkubwa kisiwani hapo kwa shughuli za maendeleo na kuishukuru serikali kwa mradi huo.
Juma Hamisi mkazi wa kisiwa hicho amesema wamekuwa wakifanyia shughuli za uchomereaji nje ya kisiwa hicho na kutumia gharama kubwa na kumshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwa mfatiliaji wa miradi ya maendeleo.
Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema Kisiwa cha Rukuba inayo miradi mwili (2) ya umeme jua ambayo matayarisho yanafanywa na REA
Umeme jua utaungwa kwenye kituo cha afya ambapo REA imeishampata Mkandarasi na taratibu za kisheria zinakamilishwa.
Amesema umeme jua kwenye maeneo mengine ya kisiwani humo REA ina mradi kabambe wa kusambaza umeme jua kwenye visiwa vyote vya Ziwa Victoria na Bahari ya hindi huku wakandarasi wakitafutwa
Muhongo amesema pampu ya maji ya kutumia umeme jua RUWASA inasubiri upatikanaji wa umemejua ili ianze kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji ya bomba hapo kisiwani.

Comments
Post a Comment