Wanafunzi wa shule ya sekondari Machimboni iliyopo Wilaya ya Mpanda,Mkoa wa Katavi wametakiwa kuepuka kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi bali waishike sana elimu kwa manufaa ya maisha yao hapo baadae.
Wito huo umetolewa Agosti 01,2024 na Polisi kata wa kata ya Machimboni Mkaguzi msaidizi wa Polisi Subiri Challi ambapo ametoa elimu ya ukatili wa kijinsia na aina zake jinsi gani wataweza kuepuka na vitendo hivyo.
Pia amewataka Wanafunzi kuepukana na vishawishi hasa kupokea zawadi Toka Kwa mtu au watu wasiowafahamu kwani baadhi ya wahalufu hutumia mwanya huo kutekeleza Vitendo Vya kihalifu.


Comments
Post a Comment