Na Mwandishi wetu-Tarime
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava, amezindua jengo la kisasa la Nyamongo Plaza lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Jengo hilo la ghorofa mbili, ni mali ya mfanyabiashara Josephat Mwita lililojengwa kwa ajili ya shughuli za kibiashara katika mji wa Nyamongo, jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.
Akizungumza mara baada ya kuzindua jengo hilo wakati wa mbio za Mwenge katika mji ndogo wa Nyamongo, Mnzava amempongeza mwekezaji huyo na kusema hatua hiyo ni kielelezo cha ushiriki wa sekta binafsi katika kuchangia ukuzaji wa uchumi nchini.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava akizindua jengo la Nyamongo Plaza. Kushoto ni mmiliki wa jengo hilo, Josephat Mwita na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Mwalimu Saul Mwaisenye.
Amempongeza mwekezaji huyo Bw Josephat Mwitakwa kazi hiyi nzuri na kusema ujenzi huo ni sehemu ya kuunga mkoni juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kafungua milango ya uwekezaji na biashara nchini.
Amesema kuwa kujengwa kwa jengo hilo litawezesha halmashauri kupata kupata kukusanya mapato mbalimbali, huku serikali kuu kuweza kukusanya kodi mbalimbali ambazo zitaelekezwa kwenye huduma za jamii.
Aidha, Mnzava amemkabidhi mfanyabiashara huyo Josephat Mwita Mwenge wa Uhuru kama ishara ya serikali kutambua ushiriki wake katika uwekezaji na biashara kupitia sekta binafsi.
Josephat Mwita ni moja ya wananchi wachache wa mkoa wa Mara,ambao wamejitokeza kuwekeza katika maeneo wanayotoka,ambapo mbali na kujenga jengo hilo hilo pia amekuwa akijihusisha na kilimo cha Alizeti na shughuli za uchimbaji wa madini ingawa baadhi ya watu wasipenda maendeleo wamekuwa wakihujumu jitihada zake hizo za maendeleo mkoani Mara.
Akiwa katika eneo hilo Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, pia amejionea uendelevu wa mradi mkubwa wa majisafi na salama ya bomba uliotekelezwa chini ya usimamizi wa RUWASA katika kijiji cha Nyangoto, Nyamongo kutokana na fedha za Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kutoka mgodi wa Noth Mara.






Comments
Post a Comment